Walinda Amani Wapelekwa Afrika Ya Kati Kulinda Uchaguzi

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito kwa pande zote kukomesha haraka vitendo vya uhasama katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, wakati nchi hiyo ikielekea katika uchaguzi wa rais Desemba 27.

Msemaji wa Guterres, Stephane Dujarric amesema mkuu huyo wa Umoja wa Mataufa amelaani ongezeko la machafuko na kuzitaka pande zote kufanya kazi ya kuhakikisha kuna mazingira bora ya kuandaa uchaguzi halali, unaozijumuisha pande zote na wenye amani mnamo Desemba 27.

Makundi matatu makuu ya wapiganaji ambayo yanadhibiti thuluthi mbili ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yamemtishia Rais Faustin Archange Touadera, yakimtuhumu kwa kupanda wizi wa kura ili kushinda muhula wa pili.


EmoticonEmoticon