Wanahabari Wasio Na Vyeti Vya Kuangazia Uchaguzi Wazuiwa Uganda

Wanahabari wasiokuwa na idhini ya kuangazia uchaguzi mkuu wa Uganda wamezuiliwa kufanya hivyo.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano usiku na Inspekta Jenerali wa polisi nchini humo, Meja Jenerali Paul Lokech amesema agizo hilo litaanza kutekelezwa kuanzia Desemba 31.

Lokech amesema polisi wote na mashirika ya usalama yatawatambua wanahabari ambao wameidhinishwa na Baraza la Habari la Uganda kuangazia shughuli za kampeni na uchaguzi.

Taarifa yake inajiri saa kadhaa baada ya kukamatwa kwa mabloga kadhaa na wachapishaji wengine wa mtandaoni wanaohusishwa na chama cha upinzani cha National Unity Party ambao walikuwa wakiangazia kuzuiliwa kwa kampeni za Bobi Wine na kukamatwa kwa maafisa wa kampeni zake katika wilaya ya kati ya Kalangala. 


EmoticonEmoticon