Wasomali Wamuomba Biden Kubadili Uamuzi Wa Trump Kuondoa Majeshi

 

Uamuzi wa Rais Donald Trump kuwaondoa wanajeshi wa Marekani nchini Somalia katika siku za mwisho za urais wake, umechochea malalamiko kutoka kwa baadhi ya Wasomali, ambao wamemuomba rais ajaye Joe Biden kubadili uamuzi huo.

"Uamuzi wa Marekani kuondoa wanajeshi wake nchini Somalia katika kipindi hiki muhimu cha mafanikio katika mapamano dhidi ya al-Shabaab na mtandao wao wa kigaidi ulimwenguni ni jambo la kusikitisha sana,” Seneta Ayub Ismail Yusuf ameliambia shirika la habari la Reuters katika taarifa, akilitaja al-Qaeda likihusishwa na uasi wa al-Shabaab.

"Wanajeshi wa Marekani wamekuwa na mchango mkubwa na mafanikio mazuri katika mafunzo na operesheni kwa wanajeshi wa Somalia,” amesema Yusuf, mjumbe katika kamati ya mambo ya nje kwenye baraza la senate la Somalia.

Serikali ya Somalia haikuweza kupatikana haraka kutoa maoni yake mapema Jumamosi kuhusu uamuzi wa Ijumaa wa kuondoa takriban wanajeshi wote 700 wa Marekani ifikapo Januari 15.


EmoticonEmoticon