Watoto Watumika Kama Wapiganaji Mali

 

Ripoti ya mashirika ya kibinadamu yakiongozwa na shirika la umoja wa mataifa la kuwashughulikia wakimbizi UNHCR, imenakili visa 230 vya Watoto kusajiliwa na makundi ya wapiganaji katika miezi sita ya kwanza ya mwaka 2020, ikilinganishwa na visa 215 mwaka 2019.

Mashirika hayo pia yamesema kwamba Watoto 6,000 wengi wao wakiwa wavulana, wanafanya kazi katika machimbo ya dhahabu.

Msaidizi wa mkuu wa UNHCR Gillian Triggs, amesema kwamba vita na hali mbaya ya uchumi kutokana na janga la Corona katika eneo la Sahel imesababisha ukiukwaji mkubwa wa haki za kibinadamu eneo hilo.

Amesema kwamba Watoto wanasafirishwa kimagendo, kunajisiwa, kuuzwa, kulazimishwa kufanya ngono au kulazimishwa kuoa na kuolewa.


EmoticonEmoticon