Karibu watu
13 wameuawa katika milipuko miwili inayo ripotiwa kuutikisa uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Aden, kusini mwa Yemen, Jumatano muda mfupi tu baada ya kuwasili
ndege iliyokuwa ina wasafirisha wajumbe wa serikali mpya ya umoja wa kitaifa.
Ingawa hakuna kati ya maafisa hao wa serikali waliojeruhiwa
lakini ina ripotiwa kuna zaidi ya watu 50 waliojeruhiwa na huenda idadi ya vifo
ikaongezeka.
Haijafahamika mara moja kilicho sababisha milipuko hiyo
lakini milio ya bunduki ya hapa na pale ilisikika karibu na uwanja huo.
Serikali ya Yemen inayotambulika kimataifa na wapiganaji
wanaotaka kujitenga huko kusini wameunda serikali mpya ya pamoja kushirikiana
madaraka hapo Disemba 18 na waliwasili katika mji huo wa kusini wa Aden
Jumatano baada ya kuapishwa nchini Saudi Arabia.
Serikali hiyo ya wajumbe 24 iliundwa chini ya usimamizi wa
serikali ya Riyadh ambayo inaongoza muungano wa nchi za Kiarabu unaopambana na
Wahouthi wanaoungwa mkono na Iran wanaoshikilia mji mkuu wa Sanaa tangu 2014.
Serikali hiyo mpya iliyoapishwa na rais Abderabbo Mansour siku ya Jumamosi imeundwa kupambana na uasi unaoendelea katika sehemu kubwa ya kaskazini mwa nchi.
Credit:Voa
EmoticonEmoticon