WhatsApp Haitofanya Kazi Mwaka 2021 Kwa Matoleo Haya Ya Simu

 

WhatsApp haitafanya kazi 2021 katika simu kadhaa zinazotumia Android na iOS. Sababu zikiwa ni za kiusalama na za kiteknolojia.

Ni kawaida kila baada ya miaka kadhaa kwa WhatsApp kuacha kufanya kazi au kutotolewa kwa matoleo mapya/masasisho kwa baadhi ya simu.

Mara nyingi sababu kuu huu ni simu hizo kufikia mwisho wa kupokea masasisho (updates) ya programu endeshaji (os).

Kwa iPhones

Simu za iPhone zinazotumia programu endeshaji ya iOS ya chini ya toleo la 9 (iOS 9) zote zitakosa kupata app ya WhatsApp tena. Kwa sasa hii ina maanisha simu za iPhone 4 na nyingine zote zilizotoka kabla yake.

Kwa watumiaji wa simu za 4S, 5, 5S, 5C, 6 na 6S watatakiwa kuhakikisha wanatumia toleo la iOS 9 au jipya zaidi ili kuweza kuendelea kutumia app hii maarufu ya mawasiliano.

Kwa simu za Android

Kama simu unayotumia ina toleo la Android la 4.0.2 na nyuma basi itakuwa ndio mwisho wa kuweza kutumia app ya WhatsApp. Simu ambazo hazina uwezo wa kupata toleo la Android la juu zaidi ya hapo ni pamoja na HTC Desire, Motorola Droid Razr, na Samsung Galaxy S2. Simu hizi hazitakuwa na uwezo tena wa kutumia app ya WhatsApp.


EmoticonEmoticon