WHO Yatathmini Chanjo Ya Pfizer ili Kuanza Kutumika Kwa Dharura

 

Shirika la Afya Ulimwenguni - WHO limesema kuwa limepokea data kutoka kwa kampuni za Pfizer na BioNTech kuhusu chanjo ya Covid-19 na inazitathmini kwa uwezekano wa kuiorodhesha kwa matumizi ya dharura, ili nchi nazo ziweze kuidhinisha matumizi ya kitaifa. 

Uingereza imeidhinisha leo chanjo ya Covid-19 inayotengenezwa na Pfizer, na kuzipiku Marekani na Ulaya kama nchi ya kwanza ya magharibi kuiidhinisha rasmi dawa hiyo iliyosema itaanza kutolewa wiki ijayo. 

Kampuni ya BioNTech ya Ujerumani na Pfizer ya Marekani, zimesema dozi za chanjo hiyo zimeanza kutumwa Uingereza mara moja ili zianze kutumika kwa umma. 

Waziri wa Afya wa Uingereza Matt Hancock amesema dozi za mwanzo 800,000 zitatolewa kwa makundi ya kipaumbele yanayojumuisha watu wanaoishi katika makaazi ya wazee na walemavu pamoja na wahudumu wa afya.


EmoticonEmoticon