Afrika Kusini Inatarajia Dozi Za Chanjo Za Corona Wiki Ijayo

 

Afrika Kusini Jumatatu itapokea dozi milioni moja ya chanjo ya Covid-19 kutoka India wakati inapambana na virusi vipya.

Waziri wa Afya Zweli Mkhize alisema dozi za AstraZeneca zitapitia michakato ya kitaalamu wakati wa kuwasili, ikiwemo kuhakikisha ubora wake.

"Michakato hii itachukua siku zisizopungua 10 na si chini ya siku 14 kukamilisha, ambapo tutakuwa tayari kusambaza chanjo hizo kwenye majimbo yote," alisema.

Serikali ilinunua dozi ya chanjo milioni 1.5 kwa Januari na Februari, na dozi za ziada milioni 20 zinatarajiwa mwezi Juni. Afrika Kusini ndio nchi iliyoathirika zaidi na janga la corona barani Afrika.


EmoticonEmoticon