Afrika Kusini Yachelewesha Kuanza Mwaka Mpya Wa Masomo Kudhibiti COVID-19

 

Afrika Kusini Ijumaa imechelewesha kuanza kwa mwaka mpya wa masomo kwa kipindi cha wiki 2 hadi Februari 15, ili kuzizuia shule zisiwe vituo vya maambukizi ya covid 19.

Wakati huohuo kumeripotiwa kesi mpya za maambukizi 20,000 kwa siku wiki iliyopita.

Shule zilifungwa kwa karibu theluthi moja ya mwaka wa masomo mwaka 2020, wakati Afrika Kusini iliposhuhudia wimbi la kwanza la maambukizi ya virusi vya Corona.

“Baraza la mawaziri wa elimu limechukua uamuzi huu mgumu kwa kuzingatia mambo yote, kuhusu hali ya sasa ya mfumo wa sasa,” naibu Waziri wa Elimu ya Msingi Reginah Mhaule ameuambia mkutano wa waandishi wa habari mjini Pretoria.

“Tunatakiwa kulinda maisha ya walimu na wanafunzi”, ameongeza.

Afrika Kusini imekwisha ripoti zaidi ya vifo 35,000 kutokana na covid 19, ikiwa ni idadi ya juu barani Afrika.


EmoticonEmoticon