Aweka Mwili Wa Mama Yake Kwenye Jokofu Kwa Miaka Kumi Nchini Japani

 

Polisi nchini Japan wamemkamata mwanamke mmoja baada ya mwili wa mama yake kukutwa kwenye jokofu nyumbani kwake.

Yumi Yoshino, 48, amesema kuwa alimkuta mama yake akiwa amefariki kisha aliuficha mwili wake miaka 10 iliyopita kwa sababu '' hakutaka kuhama'' katika nyumba waliokuwa wakiishi mjini Tokyo, vyombo vya habari vimewanukuu maafisa polisi ambao hawakutajwa majina yao.

Hakukuonekana majeraha yoyote kwenye mwili ulioganda barafu, polisi wameeleza.

Mamlaka hawakuweza kuthibitisha muda na sababu ya kifo cha mwanamke huyo.

Mwili uliripotiwa kugundulika na mfanya usafi baada ya Bi. Yoshino kulazimishwa kuondoka katika nyumba hiyo kwa sababu ya kukosa kodi.

Mwili ulikuwa umekunjwa kiasi cha kutosha kuingia kwenye jokofu lenye barafu, polisi walisema.

Bi Yoshino alikamatwa katika hoteli mjini Chiba karibu na jiji la Tokyo, siku ya Ijumaa.


EmoticonEmoticon