Baraza la Seneti la Bunge la Marekani Lamuidhinisha Waziri Wa Fedha

 

Baraza la Seneti la Bunge la Marekani limepiga kura na kumuidhinisha kwa wingi mkubwa mwanauchumi anayeheshimika Janet Yellen kuwa Waziri wa Fedha wa Taifa hilo.

Wajumbe wa Seneti wamemuidhinisha Yellen kwa kura 84 za ndio dhidi ya 15 za hapana na kumfanya kuwa Mwanamke wa kwanza kuongoza Wizara hiyo tangu ilipoanzishwa zaidi ya miaka 200 iliyopita.

Yellen anatajwa kuwa miongoni mwa wachumi wenye tajriba kubwa baada ya hapo kabla kufanya kazi kama Gavana wa Benki Kuu ya Marekani na Mjumbe wa Baraza la Washauri wa Uchumi wa Ikulu ya White House.


EmoticonEmoticon