Baraza La Seneti Lapokea Mashtaka Dhidi Ya Trump

 

Baraza la Wawakilishi la Bunge la Marekani limewasilisha hati ya mashtaka mbele ya Baraza la Seneti dhidi ya rais wa zamani Donald Trump na kufungua njia ya kuanza kwa shauri la pili la kihistoria. 

Wawakilishi tisa walioteuliwa kuongoza mchakato huo wamewasilisha shtaka moja pekee linalomtuhumu Trump "kuchochea uasi" baada ya wafuasi wake kuvamia majengo ya Bunge mjini Washington mapema mwezi huu.

Wakitembea kwa mwendo wa polepole wawakilishi hao waliwasilisha hati ya mashtaka mbele ya Baraza la Seneti na kufungua njia ya kuanza kwa shauri la kihistoria kwa kiongozi wa taifa hilo kushtakiwa mara mbili na Bunge.

Mwakilishi wa jimbo la Maryland Jamie Raskin  ndiye alisoma shakta dhidi ya Trump ndani ya ukumbi wa Baraza la Seneti, ambako rais huyo mstaafu bado uungwaji mkono kutoka maseneta wa chama chake cha Republican.

Kuwasilishwa kwa hati hiyo ya mashtaka iliyoidhinishwa na Baraza la Wawakilishi linaloongozwa na chama cha Democrat mnamo Januari 13 kunafungua njia ya kuanza kwa shauri dhidi ya Trump katika wiki ya pili ya mwezi Februari.


EmoticonEmoticon