Baraza la
Seneti la Marekani linatarajiwa kukutana Ijumaa kupiga kura ya kumuidhinisha
Jenerali mstaafu Lloyd Austin aliependekezwa na rais Joe Biden kwenye wadhifa
wa Waziri wa Ulinzi.
Alhamisi Baraza la Wawakilishi na Seneti walipitisha kanuni
ya kisheria kumruhusu Austin kuchukua wadhifa wa waziri wa ulinzi kama raia wa
kawaida chini ya miaka 7 tangu ajiuzulu kwenye jeshi la Marekani.
Austin ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Vikosi vya Marekani
Mashariki ya Kati na Asia kusini na Kamanda wa Uongozi wa jeshi, akiidhinishwa
na Seneti, atakuwa Mmarekani mweusi wa kwanza kuchukua wadhifa wa Waziri wa Ulinzi.
Baraza la Seneti linatarijiwa pia kumuidhinisha Balozi wa zamani William Burns aliependekezwa na Rais Biden kuongoza idara ya Ujasusi ya Marekani, CIA.
EmoticonEmoticon