Rais Joe
Biden wa Marekani ameomba msamaha baada ya baadhi ya wanajeshi waliokuwa
wamewekwa kulinda eneo la Capitol kupigwa picha wakiwa wamelala katika eneo la
kuegesha magari.
Zaidi ya wanajeshi 25,000 walipelekwa Washington DC kwa ajili
ya kushughuli ya kuapishwa kwake mapema mwezi huu.
Picha walizopigwa maafisa hao zilianza kusambaa mtandaoni
Alhamisi zikiwaonesha wakiwa wamepumzika katika eneo la karibu la kuegesha
magari wabunge waliporejea.
Hali hiyo ilisababisha hasira miongoni mwa wanasiasa huku baadhi
ya magavana wakawaondoa wanajeshi wao kwasababu ya utata huo.
Bwana Biden
alizungumza na mkuu wa jeshi la kulinda usalama wa taifa Ijumaa, kuomba msamaha
na kuuliza ni kipi ambacho kingekuwa kimefanywa kuweka mambo sawa, kulingana na
vyombo vya habari vya Marekani.
Mama wa taifa Jill Biden pia naye alitembelea baadhi ya
vikosi hivyo kuwashukuru akiwa amewabeba biskuti kutoka Ikulu kama zawadi.
"Leo hii nilitaka tu kuja na kuwashukuru kwa kutulinda
mimi pamoja na familia yangu," alisema.
Picha hizo zinazoonesha mamia ya wanajeshi wakiwa eneo la kuegesha magari zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii Alhamisi na kusababisha hasira.
EmoticonEmoticon