Bunge Lamuidhinisha Joe Biden Kuwa Mshindi Wa Uchaguzi Wa Urais Marekani

 

Bunge la Congres limemuidhinisha Joe Biden na Kamala Hariss kama rais mtarajiwa na makamu wake wa Marekani.

Bunge hilo liliwaidhinisha wawili hao kwa kura 282 huku wabunge 138 wakipiga kura ya kupinga matokeo ya jimbo la Pennsylvania. Bunge la seneti lilikataa pingamizi kama hiyo.

Kura za wajumbe zilithibtishwa baada ya mabunge yote mawili lile la uwakilishi na lile la seneti kukataa pingamizi kuhusu kura zilizopigwa katika vituo vya jimbo la Pennsylvania na Arizona.


EmoticonEmoticon