China
imeanza kutumia aina mpya ya kuchukua sampuli za kipimo Cha Corona kupitia
sehemu ya haja kubwa.
Mamlaka zinasema aina hii ya kipimo
ni ya kuaminika zaidi na haraka.
Kipimo hiki kinahusisha kuingiwa kwa
kifaa maalumu chenye pamba kama sentimita 1 ama 2 katika njia ya haja kubwa
kisha kutoa sampuli ambayo itatumika kuangalia uwepo wa virusi vya Corona.
Kwa mujibu wa televisheni ya taifa
hilo CCTV inasema kuwa aina hii ya kipimo itatumika kwa visa vitakavyo hitaji
uangalizi wa hali ya juu.
Watu ambao watapimwa na kipimo hiki
ni pamoja na abiria watakaoingia Beijing na watu watakaokuwa wamewekwa
karantini.
“Kipimo hiki kina ufanisi zaidi
kuliko kile Cha puani na kwenye koo” Anasema Li Tongzeng afisa msaidizi katika
kitengo Cha mfumo wa upumuaji katika hospitali ya You an.
Hatua hii inakuja kama maandalizi ya kupambana na Corona wakati wa sherehe za mwaka mpya wa China
EmoticonEmoticon