Wasimamizi
wa sekta ya afya nchini China wamesema kwamba wameidhinisha chanjo dhidi ya
virusi vya Corona ambayo imetengenezwa na kampuni inayomilikiwa na serikali ya
Sinopharm.
Naibu wa
kamisaa wa tume ya usimamizi wa dawa nchini China Chen Shifei, ameambia
waandishi wa habari mjini Beijing kwamba hatua hiyo imefanyika jana usiku.
Chanjo hiyo
ya dozi mbili ni ya kwanza kuidhinishwa kwa matumizi ya kawaida nchini China.
Hatua hiyo
inajiri wakati nchi hiyo inaendelea kufanya kampeni ya kutoa chanjo kwa watu milioni
50 kabla ya maadimisho ya mwaka mpya nchini China, unaoadhimishwa mwezi
Febrauri.
Chanjo hiyo
imetengenezwa na taasisi ya biolojia ya Beijing, ambayo sehemu yake inamilikuwa
na kampuni ya Sinopharm.
Kampuni hiyo
imesema kwamba utafiti wa awali unaonesha kwamba chanjo yake ina ufanisi wa
asilimia 79.3.
Kampuni ya Sinopharm ni mojawapo ya kampuni za kutengeneza dawa nchini China, ambazo zinatengeneza chanjo dhidi ya virusi vya Corona, ambavyo vimeua zaidi ya watu milioni 1.8 kote duniani.
EmoticonEmoticon