China Yaipiku Marekani Na Kuchukua Nafasi Ya Kwanza Kama Kivutio Cha Uwekezaji Wa Kigeni Duniani

 

China imeipiku Marekani kama eneo linalolengwa na uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni kulingana na takwimu za UN zilizotolewa siku ya Jumapili.

Nusu ya uwekezaji mpya nchini Marekani kutoka katika makampuni ya kigeni ulishuka mwaka uliopita hatua iliosababisha taifa hilo kupoteza nafasi yake ya kwanza.

Kwa upande mwingine, takwimu hizo zinaonyesha uwekezaji wa moja kwa moja katika kampuni za Wachina uliongezeka kwa asilimia 4 , na kulifanya taifa hilo kuchukua nafasi ya kwanza duniani.

Kupanda kwa China kunaonesha ushawishi wake katika sekta ya kiuchumi duniani.

China ilijipatia kipato cha $163bn (£119bn) mwaka uliopita , ikilinganishwa na $134bn zilizoingia Marekani, Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na Maenedeleo (UNCTAD) ulisema katika ripoti yake.


EmoticonEmoticon