Mshambuliaji
wa Juventus Cristiano Ronaldo anachunguzwa na maafisa wa polisi wa Itali kuhusu
safari aliokwenda ili kusherehekea siku ya kuzaliwa na mpenzi wake.
Anatuhumiwa kwa kuvunja masharti ya Covid -19 kwa kusafiri
kati ya jimbo la Piedmont na Valle d'Aosta.
Picha zilizochapishwa na baadaye kuondolewa mtandaoni
zinawaonesha wawili hao wakiwa katika hoteli moja siku ambayo Georgina
Rodriguez alisherehekea kua na umri wa miaka 27.
Italy imeshuhudia mamia ya vifo na maelfu ya maambukizi mapya
kila siku.
Taifa hilo
liliathiriwa vibaya mapema wakati wa mlipuko huo mwaka uliopoita na sasa liko
katika mzozo wa ksiasa baada ya kushindwa kupunguza idadi maambukizi katika
wimbi la pili la maradhi hayo.
Maafisa wa polsi wa Valle d'Aosta wanasema kwamba wanawachunguza
wapenzi hao kuhusu safari hiyo ya mgahawa wa Courmayeur ski
Chini ya sheria zilizopo nchini Itali, safari kati ya maeneo
yenye maambukizi ya Corona zimepigwa marufuku isipokuwa iwapo ni ziara ya
kikazi ama kwenda nyumbani
Ripoti nchini Itali zinadai kwamba wawili hao walisafiri siku
ya Jumanne na kusalia katika mgahawa huo usiku kucha kabla ya kurudi Turin,
nyumbani kwa klabu ya Serie A Juventus siku ya Jumatano.
Endapo watapatikana wamekiuka sheria huenda wote wakapigwa faini.
EmoticonEmoticon