Democrats Wajiandaa Kuchukua Hatua Dhidi Ya Ghasia Za Capitol Hill Kwa Kumshtaki Trump

 

Bunge La wawakilishi nchini Marekani huenda likapiga kura mapema siku ya Jumanne kuhusu kifungu cha sheria cha kumshtaki rais Donald Trump, afisa mkuu wa chama hicho amesema.

Wabunge wa Democrats wanapanga kumshtaki bungeni rais Trump kwa 'malipo ya uasi' dhidi ya hatua yake ya 'kuchochochea ghasia' zilizosababisha uvamizi wa jumba la Bunge la Capitol Hill.

Kiranja wa bunge James Clyburn aliambia CNN kwamba hatua zitachukuliwa wiki hii.

Lakini chama hicho huenda kisitumie kifungu chochote cha sheria katika bunge la seneti ili kumfungulia mashtaka hayo hadi rais mteule Joe Biden atakapohudumu siku zake 100 za kwanza afisini.

''Tumpatie rais Mteule Joe Biden siku 100 za kwanza ili aanzishe ajenda yake ya utawala'', alisema bwana Clyburn.

Hatua hiyo itamruhusu bwana Biden kuthibitisha baraza lake jipya la mawaziri na kuanzisha sera muhimu ikiwemo kukabiliana na virusi vya corona kitu ambacho kitalazimika kusubiri iwapo bunge la seneti litakuwa limepokea vifungu hivyo vya kumshtaki rais Donald Trump.

Bwana Trump hajatoa taarifa yoyote kwa umma tangu alipofungiwa na baadhi ya mitandao ya kijamii ikiwemo Twitter siku ya Ijumaa.


EmoticonEmoticon