EU Yapendekeza Kuimarishwa Mipaka Kutokana Na Kitisho Cha Corona

 

Halmashauri Kuu ya Ulaya imependekeza kuwa mataifa yote ya Umoja wa Ulaya yaimarishe mipaka yao, na kuwataka wasafiri kutoka nchi zisizo mwanachama wa umoja huo kuwasilisha vipimo vyao vya kuonyesha kuwa hawana maambukizi ya virusi vya corona ambavyo vina chini ya saa 72 kabla ya kuanza safari yao.

Kamishna wa Sheria wa Umoja wa Ulaya Didier Reynders amesema leo kuwa ipo haja ya dharura ya kupunguza kitisho cha maambukizi kinachohusiana na usafiri ili kupunguza mzigo wa mifumo ya afya iliyoelemewa.

Amesema kuna viwango vikubwa vya maambukizi katika mataifa mengi wanachama.

Serikali ya Ujerumani imesema leo kuwa ina wasiwasi kuhusu maambukizi ya aina mpya ya kirusi cha corona kilichogundulika kwa mara ya kwanza Uingereza.

Msemaji wa serikali Steffen Seibert amesema kirusi hicho kinaweka hatari kubwa nchini, ambapo mpaka sasa kuna idadi ndogo ya visa vilivyogundulika. Amesema maambukizi ya virusi vya corona yameanza kupungua kutokana na hatua zilizowekwa na serikali.


EmoticonEmoticon