Shirika la
upelelezi la Marekani FBI, limeonya kuhusu uwezekano wa maandaamnao yenye
silaha kufanywa kote nchini siku chache kabla ya Joe Biden kuapishwa kuwa rais.
Kuna ripoti ya makundi yaliojihami yanapanga kukusanyika
katika mabunge ya majimbo yote 50 na Washington DC kuelekea siku ya kuapishwa
kwake Januari 20.
Hofu hiyo inajiri wakati mipango ya usalama imeimarishwa kwa
ajili ya hafla hiyo.
Siku ya Jumatatu Bw. Biden aliwaambia wanahabari kwamba
haogopi kula kiapo chao urais nje ya bunge la Marekani.
Yeye pamoja
makamu wake mteule Kamala Harris bado wanatarajiwa kuapishwa nje ya jumba la
Capital Hill, wiki mbili baada ya eneo hilo kuvamiwa na wafuasi sugu wa Rais
Trump wanaopinga matokeo ya uchaguzi.
Maafisa wa usalama wamesisitiza hali iliyoshuhudiwa Januari 6 haitarudiwa tena- baada ya maelfu ya wafuasi wa Trump kufanikiwa kuingia katika majengo hayo wakati wabunge walikuwa wakipiga kura kuidhinisha matokeo ya uchaguzi.
EmoticonEmoticon