Frank Lampard Afutwa Kazi Ya Ukocha Chelsea

 

Chelsea imemfuta kazi kocha wake Frank Lampard baada ya kuingoza klabu hiyo kwa miezi 18.

Lampard, 42, ambaye ni kuingo wa zamani wa klabu hiyo, anaiacha Chelsea katika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi ya Primia huku wakishinda mechi moja tu ya ligi kati ya tano zilizopita. Mchezo wao wa mwisho wa ligi kuu wiki iliyopita walifungwa na Leicester City.

Mechi yake ya mwisho kama kocha wa miamba hiyo ya London ulikuwa Jumapili wakishinda 3-1 dhidi ya Luton kwenye michuano ya FA.

Kocha wa zamani wa Paris St-Germain na Borussia Dortmund Thomas Tuchel anatarajiwa kutua katika dimba la Stamford Bridge kurithi nafasi ya Lampard.


EmoticonEmoticon