Mamia ya
vijana Jumatatu wamekusanyika kwenye miji tofauti yaTunisia wakati baadhi
wakirusha mawe na mabomu ya kujitengenezea, kwenye mji mkuu wa Tunis, wakati
maafisa wa usalama wakijaribu kutuliza hali kwa kutumia gesi ya kutoa machozi
pamoja na maji.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, hadi vijana 300
walikabiliana na polisi kwenye kitongoji cha Ettadamon kilichoko Tunis wakati
wakazi kwenye miji ya Kasserine,Gafsa,Sousse na Monastir wakidai kushuhudia
ghasia.
Ghasia hizo zimetokea wakati wa maadhimisho ya miaka 10 tangu
mapinduzi yalioleta demokrasia ingawa wakazi wengi wa Tunisia wanalamika kuwa
hakuna kilichobadilika. Umasikini pamoja na ukosefu wa ajira zinasemekana
kuongezeka kwa kiasi kikubwa.
Haijabainika iwapo maandamano hayo yataendelea kwa muda au
yatamalizika kutokana na kuwa hayaungwi mkono na chama chochote cha kisiasa,
kinyume na yale yalioshuhudiwa miaka ya nyuma.
Shirika la kutetea haki za binadamu lenye makao yake mjini
London la Amnesty International limeomba maafisa usalama kuwa wapole wakati likionyesha
video fupi ya waandamanaji wakikamatwa na kuzuiliwa.
Limeomba pia kuachiliwa mara moja kwa mwanaharakati wa haki za binadamu Hamza Nassri Jeridi aliezuliwa Jumatatu. Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani amesema Jumatatu kuwa polisi walizuilia watu 632 Jumapili pekee, kwa kile kimetajwa kuwa uharibifu na wizi wa mali wakati wa maandamano. Wengi wa waliozuiliwa wanasemekana kuwa na umri kati ya kumi na tano na ishirini.
EmoticonEmoticon