Tetesi Za Soka Ulaya Jumatatu January 11, 2021
1. Napoli wameamua kumfanya mlinzi
wa Arsenal Mskochi Kieran Tierney lengo lao la muda mrefu baada ya kumkosa
nyota huyo aliye na umri wa miaka 23 mwanzo wa msimu huu.
2. Manchester United inajiandaa
kumenyana na Paris St-Germain katika mbio za kumsaka kiungo wa kati wa Brest na
Ufaransa mwenye chini ya miaka 21 Romain Faivre.
3. Chelsea hawako tayari
kumuachilia kiungo wa kati wa England Ross Barkley kujiunga na Aston Villa -
ambako anacheza kwa mkopo wa msimu mzima -huku mchezaji huyo mwenye umri wa
miaka 27 akisalia na miaka miwili na nusu kwenye mkataba wake.
4. Winga wa England Jadon Sancho
amekiri kwabma amekuwa na msimu mgumu Borussia Dortmund tangu alipohusishwa na
tetesi za kujiunga na Manchester United, lakini nyota huyo wa miaka 20-
anaamini kuwa amerejelea hali yake ya kawaida.
5. Wakala wa kiungo wa kati wa Manchester City Fernandinho amegusia uwezekano wa mchezaji huyo aliye na umri wa miaka 35- kurejea klabu ya Brazil ya Athletico Paranaense mkataba wake na City utakapomalizika.
EmoticonEmoticon