Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa January 1, 2021
1. Manchester United imemuongezea
kandarasi ya mwaka mmoja kiungo wa kati wa England Jesse Lingard na sasa
kandarsi ya mchezaji huyo itakamilika 2022.
2. Arsenal inajianda kumnunua
kiungo wa kati wa Real Madrid na Uhispania Isco kwa kipindi cha msimu uliosalia
, lakini wanasubiri kuona iwapo klabu hiyo ya Uhispania itamwachilia mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 28 katikati ya kampeni yao.
3. Liverpool imeanza mazungumzo na
ajenti wa Sven Botman, ambaye anataraji kwamba the Reds watawasilisha ombi la
kumnunua mchezaji wa Lille na Uholanzi anayechezea timu ya wachezaji wasiozidi
umri wa miaka 20.
4. Beki wa Uhispania Eric Garcia,
19, ameafikiana na klabu ya Barcelona kujiunga na mibabe hiyo ya La Liga katika
mkataba wa miaka mitano kufuatia kukamilika kwa kandarasi yake na Manchester
City mwezi Juni na Barcelona huenda wakakamilisha uhamisho huo mwezi Januari.
5. Chelsea imejiunga na AC Milan na Nice katika kuonyesha hamu ya kutaka kumsajili beki wa Ufaransa na Strasbourg Mohamed Simakan, 20.
EmoticonEmoticon