Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa January 22, 2021
1. Leicester City wameacha mpango
wao wa uhamisho kwa ajili ya kiungo wa kati wa Inter Milan Christian Eriksen,
28, kwasababu mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark anataka mshahara wa pauni
300,000-kwa wiki.
2. Bayern Munich wamethibitisha
haja yao ya kusaini mkataba na Mlinzi wa RB Leipzig Mfaransa Dayot Upamecano,
mwenye umri wa miaka 22 ambaye katika mkataba wake ana kipengele cha
kumuachilia cha thamani ya pauni milioni 40.
3. Manchester United, Manchester
City na Chelsea kwa pamoja wameonesha nia yao katika ya kumtaka Dayot
Upamecano, ambaye mkataba wake hautasainiwa hadi mimu ujao.
4. Arsenal wanataka kusaini
mkataba na kiungo wa kati- kushoto Mskochi Kieran Tierney, 23, kabla ya
kumalizika kwa dirisha la uhamisho wa wachezaji mwezi Januari.
5. Kiungo wa kati wa Tottenham na England Dele Alli, 24, amemuomba mwenyekiti Daniel Levy asimuwekee pingamizi katika uwezekano wke wa kuhamia Paris St-Germain.
EmoticonEmoticon