Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa January 29, 2021
1. Paris St-Germain itafirikia
kumuuza mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, mwisho wa msimu huu iwapo
mshindi huyo wa kombe la dunia atakataa kuandikisha kandarasi mpya na klabu
hiyo. Klabu ya Liverpool na ile ya Real Madrid zina hamu ya kumsaini mshambuliaji
huyo hatari.
2. Chelsea ina hamu ya kumsaini
mshambuliaji wa Borrusia Dortmund mwenye umri wa miaka 20 Erling Haaland Kutoka
klabu ya Borussia Dortmund pamoja na beki wa Bayern Munich raia wa Austria
David Alaba, 28, mwisho wa msimu huu .
3. West Ham Itabadilisha kandarasi
ya mkopo ya kiungo mshambuliaji wa Algeria Said Benrahma kutoka Brentford na
kumsajili kwa kandarasi ya kudumu. West ham ililipa dau la £4.25m kumnunua
mchezaji huyo kwa mkopo na italipa dau la £21.75m kumnunua mchezaji huyo.
4. Mkufunzi wa Arsenal Mikel
Arteta amesema kwamba atafikiria uwezekano wa kuongeza muda wa kandarasi ya
mkopo ya Martin Odegaard ili kusalia katika klabu hiyo zaidi ya msimu huu baada
ya kujiunga na klabu hiyo kutoka Real Madrid.
5. Mkufunzi mpya wa Chelsea Thomas Tuchel hana mpango wa kuwasajili wachezaji wapya katika kipindi kilichosalia cha dirisha la uhamisho.
EmoticonEmoticon