Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa January 8, 2021
1. Menega wa klabu ya Fernabahce
Erol Bulut amesema kwamba hali kuhusu uwezekano wa klabu hiyo kumsaini kiungo
mchezeshaji wa Arsenal na Ujerumani Mesut Ozil 32 itakuwa wazi katika siku
chache zijazo ".
2. Manchester City inakaribia
kumsaini 'Messi mdogo' Dario Sarmiento. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17
winga wa Argentina anaichezea klabu ya Estudiantes katika ligi ya nchi hiyo.
3. Mkufunzi wa Burnley Sean Dyche
ametaka chanjo ya corona kuharakishwa katika soka huku fedha zinazohifadhiwa
kuwapima wachezaji zikiepelekwa katika idara ya afya.
4. Kiungo wa kati wa Man United na
Uholanzi Donny van de Beek huenda akaondoka kulingana na mshambuliaji wa zamani
wa klabu hiyo Dimitar Berbatov. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23
ameanzishwa katika mechi mbili za ligi msimu huu baada ya kusainiwa kwa dau la
£35m mwezi Septemba.
5. Newcastle pia imewasilisna na Monaco kuhusu beki wa Ufaransa Djibril Sidibe, 28.
EmoticonEmoticon