Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumanne January 12

Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne January 12, 2021

1. Mshambuliaji wa Ufaransa na Lyon Moussa Dembele, 24, anakaribia uhamisho wa kuelekea Atletico Madrid baada ya kukataa uhamisho wa West Ham. 

2. Tottenham huenda ikamsajili beki mwenye umri wa miaka 22 raia wa Brazil Eder Militao - anayesakwa na Roma, AC Milan na Inter - kwa mkopo kutoka Real Madrid ikiwa na mbadala wa kumnunua kwa mkataba wa kudumu.

3. Klabu ya Jose Mourinho Tottenham Hotspurs imejiunga na Leeds na Juventus katika kumsaka winga wa klabu ya Stuttgart Nicolas Gonzalez, 22, huku mchezaji huyo wa Argentina akilengwa katika dirisha la uhamisho la majira ya joto.

4. Brighton wana imani wameishinda Newcastle United katika kumsaini kiungo wa kati wa Ecuado Moises Caicedo kutoka klabu ya Indipendiente del Valle. Kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 alikuwa akilengwa na klabu ya Man United.

5. Arsenal hailengi tena kumsajili kiungo wa kati wa Norwich Emi Buendia baada ya klabu hiyo kuweka dau la £40m kumuuza mchezaji huyo wa Argentine.  


EmoticonEmoticon