Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumanne January 19

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne January 19, 2021

1. Chelsea wanajiandaa kuvunja rekodi yao ya uhamisho kwa kumsaini mchezaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 20, msimu huu, licha ya mchezaji huyo wa Norway kutoa kifungu cha thamani ya pauni milioni 66.6 ambacho hakitatumiwa hadi 2022.

2. PSG wanatarajia uamuzi wiki hii kuhusiana na azma yao ya kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Tottenham na England Dele Alli, 24.

3. Real Madrid imekubaliana kusaini mkataba na mlinzi wa Bayern Munich kutoka Austria David Alaba, 28, katika msimu ujao. 

4. Mkurugenzi wa mchezo wa Paris St-Germain Leonardo anasisitiza kuwa klabu hiyo bado iko makini kusaini mkataba na mchezaji maarufu wa Argentina Lionel Messi, 33, ambaye mkataba wake unamalizika katika Barcelona msimu huu .

5. Mkurugenzi wa masuala ya kiufundi wa AC Milan Paolo Maldini anasema uhamisho wa deni kwa ajili ya nlinzi wa Chelsea Fikayo Tomori, 23, umekamilika lakini unaweza bado kusitishwa.


EmoticonEmoticon