Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumanne January 26

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne January 26, 2021

1. Mkufunzi wa West Ham David Moyes anamtaka kiungo wa kati wa Manchester United Jesse Lingard baada ya mkufunzi wa Red Devil Ole Gunnar Solskjaer kukubali kumruhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kuondoka kwa mkopo. 

2. Manchester United inafanyakazi ya kuzikabili klabu nyengine za Ulaya kama vile Manchester City, Barcelona na Juventus, kumsaini mchezaji mwenye umri wa miaka 18 raia wa Brazil Gabriel Veron kutoka Palmeiras. 

3. Edin Dzeko anatarajiwa kuondoka klabu ya Roma baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 raia wa Bosnia kutofautiana na mkufunzi Paulo Fonseca . 

4. Mkufunzi wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino anataraji kujiunga tena na kiungo wa kati Delle Alli. Maombi matatu ya Mabingwa hao wa Ufaransa kutaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 yamekataliwa , lakini Pochettino anaungwa mkono na klabu hiyo kuendelea kumnyatia.

5. Klabu ya ligi ya Serie A Udinese ipo katika mazungumzo na klabu ya Wolves kumsaini mchezaji wa Itali Patrick Cutrone, 23, kwa mkopo . Mshambuliaji huyo amekuwa hachezeshwi mechi katika uwanja wa Molineux tangu kuwasili kwa Willian Jose kutoka klabu ya Real Sociedad. 


EmoticonEmoticon