Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatatu January 4

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatatu January 4, 2021

1. Kazi ya ukufunzi ya Frank Lampard kama meneja awa Chelsea inakabiliwa na changamoto kubwa na sasa klabu hiyo imeanza kutafuta njia. 

2. Tottenham wameanzisha mazungumzo ya mapema na mshambuliaji Harry Kane kuhusu kuongezwa kwa kandarasi yake. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 na nahodha wa England alitia saini kandarasi ya miaka sita mwaka 2018 lakini mwenyekiti Daniel Levy anataka kufunga hamu inayowasilishwa na Manchester City pamoja na Paris St-Germain.

3. Paris St-Germain imeanza mazungumzo na Everton kubadilisha kandarasi ya mkopo ya mshambuliaji wa Itali Moise Kean kwa mkataba wa kudumu wenye thamani ya £31m. 

4. Mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala, 27, ambaye alikuwa amehusishwa na uhamisho wa Tottenham na Manchester United, atauzwa na Juventus mwisho wa msimu huu iwapo atakataa kutia saini kandarasi.

5. Mkufunzi mpya wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino ataruhusiwa kukifanyia mabadiliko kikosi chake na hiyo inamaanisha kwamba huenda akamsajili kiungo wa kati wa Tottenham na England Dele Alli.Pochettino ameawasiliana na Dele Alli, ambaye alikuwa mchezaji maarufu chini ya usimamizi wake katika klabu ya Tottenham.


EmoticonEmoticon