Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatano January 13

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano January 13, 2021

1. Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich anafiikria kumrudisha meneja wa zamani Avram Grant katika uwanja wa Stamford Bridge ili kumsaidia mkufunzi Frank Lampard. 

2. Bayern Munich inatarajiwa kumsaini beki wa Reading mwenye umri wa miaka 22 Omar Richards kwa mkataba usio rasmi wakati ambapo inasubiri kandarasi yake kukamilika katika msimu wa joto.. Everton na West Ham zilikuwa na hamu ya kumsajili.

3. Real Madrid inapanga kuwauza wachezaji sita msimu huu ili kuchangisha fedha za kumsaini mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe, 22. Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, beki wa kushoto wa Brazil Marcelo, Mshambuliaji wa Serbia Luka Jovic na wachezaji watatu wa Uhispania Isco, Dani Ceballos na Brahim Diaz ndio wachezaji wanaolengwa.

4. Kiungo wa kati Fernandinho, 35, huenda akaongeza kandarasi yake katika klabu ya Manchester City kwa kuwa hana uhakikia iwapo akubali ofa kutoka Ulaya na Marekani ya latini wakati kandarasi yake itakapokamilika mwisho wa msimu wa joto.

5. Beki wa Manchester United Timothy Fosu-Mensah, 23, anatarajiwa kuhamia katika klabu ya Bayer Leverkusen kwa dau la £1.5m baada ya kukataa kuongezewa mkataba katika uwanja wa Old Trafford.


EmoticonEmoticon