Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Alhamisi January 14

 

Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi January 14, 2021

1. Wawakilishi wa kiungo wa kati wa Manchester United na England Jesse Lingard, 28, wamefanya mazungumzo ya awali kuhusu uhamisho wake wa mkopo kwenda Nice, huku mazungumzo rasmi yakitarajiwa katika wiki ijayo.

2. Tottenham huenda ikafutilia mbali mkataba wa Danny Rose katika dirisha la uhamisho wa Januari, huku West Brom ikionesha azama ya kutaka kumnunua beki huyo aliye na umri wa miaka 30. 

3. Kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Mjerumani Mesut Ozil, 32, ameamua kuacha £7m alizotarajiwa kupokea kabla ya mwisho wa msimu huu ili afanikiwe kukatiza mkataba wake na kuondoka mwezi huu. 

4. Mlinzi wa Manchester City ana Uhispania Eric Garcia, 20, amefikia makubaliano ya kibinafsi na Barcelona, lakini uhamisho wake haujakaribia kukamilika. 

5. Meneja wa Barcelona Ronald Koeman ana imani ya kuwasajili kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, na mshambuliaji wa Lyon na Uholanzi Memphis Depay, 26 kwa mkopo msimu huu. 


EmoticonEmoticon