Tetesi Za Soka Ulaya Jumatatu January 18, 2021
1. Kiungo wa Tottenham na England
Dele Alli, 24, "anataka" kuhamia klabu bingwa ya Ufara Paris
St-Germain Lakini mazungumzo baina ya timu hizo yamekuwa magumu.
2. Klabu ya West Ham United
inapima uwezekano wa kumsajili mshambuliaji kutoka Ufaransa Gaetan Laborde, 26,
ambaye ka sasa anachezea klabu ya Montpellier.
3. Kaimu rais wa Barcelona Carles
Tusquets amependekeza kumsajili beki wa Manchester City na Uhispania Eric
Garcia, 20, kwa euro milioni 8 kwa wagombea watatu wa urais wa klabu hiyo,
lakini hakuna kinachoweza kufanyika kwa sasa kwa kuwa wote hakuwa na makubaliano.
4. Mshambuliaji wa Uholanzi
Netherlands Memphis Depay, 26, anasema yeye na mchezaji mwenzie wa klabu ya
Lyon Houssem Aouar, 22, wanataka kuhamia katika "moja ya klabu tatu kubwa
duniani." Depay amekuwa akihusishwa na klabu ya Barcelona, huku kiungo kutoka
Ufaransa Aouar anaripotiwa kunyemelewa na Arsenal.
5. Kocha wa Fulham Scott Parker anasema anataka kusajili wachezaji na kumaliza biashara ya usajili mapema katika dirisha la mwezi huu.
EmoticonEmoticon