Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Alhamisi January 21

 

Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi January 21, 2021

1. Chelsea wangependelea zaidi kumbadilisha kocha wao anayekabiliwa na ukosoaji mkubwa Frank Lampard na kumuajiri meneja wa mpito katikati ya msimu Lakini Lampard atafutwa kazi kama matokeo ya Chelsea hayataboreka haraka. 

2. Arsenal wamewasiliana na kiungo wa kati wa Real Madrid na Norway Martin Odegaard, 22. 

3. Paris St-Germain wanapanga uhamisho wa ghafla kwa ajili ya kiungo wa kati-nyuma wa Manchester City na Uhispania Eric Garcia, 20. 

4. Tottenham, West Ham na Sheffield United ni miongoni mwa klabu kadhaa ambazo zinataka kusaini mkataba na kiungo wa kati wa Manchester United na England Jesse Lingard, mwenye umri wa miaka 28 kwa mkopo .

5. Arsenal wanatarajia kutoa ofa ya mkataba wa malipo ya pauni 40,000 kwa wiki kwa kiungo wa kati Muingereza Emile Smith Rowe, 20.


EmoticonEmoticon