Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatatu January 25

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatatu January 25, 2021

1. Real Madrid huenda wakawa na hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Norway na Borussia Dortmund ,20, Erling Braut Haaland, ambaye anatakiwa na Chelsea na Man United baada mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, kusema kwamba anafurahia kusalia Paris St-Germain.

2. Arsenal imeafikia makubaliano ya kumsani kiungo wa kati wa Norway Martin Odegaard, 22, kwa mkopo kutoka kwa Real Madrid. 

3. Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer atamruhusu mshambuliaji wa England Jesse Lingard, 28, kuondoka kwa mkopo wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari lakini uamuzi wa mwisho utafanywa na bodi ya klabu hiyo ya Old Trafford . 

4. Beki wa Manchester City' na Uhispania Eric Garcia, 20, na kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30 - wote wakiwa kandarasi zao zinakamilika mwisho wa msimu huu - wanalengwa na Barcelona licha ya mkufunzi wa klabu hiyo Ronald Koeman kukiri kwamba timu hiyo haipo katika nafasi ya kusajili wachezaji mwezi huu .

5. Newcastle United inatarajiwa kuthibitisha uteuzi wa Graeme Jones kuwa kocha kumsaidia wa Steve Bruce, ambaye ameunga mkono usajili huo. 


EmoticonEmoticon