Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano January 27, 2021
1. Klabu ya Tottenham imewasiliana
na kiungo wa kati wa PSG na Argentina Angel di Maria kuhusu uhamisho wa kwenda
London. Mchezaji huyo wa zamani wa Man United mwenye umri wa miaka 32
anapatikana kwa uhamisho wa bila malipo mwisho wa msimu huu.
2. PSG bado inatumai kumsajili
kiungo wa kati wa Tottenham na England Dele Alli, 24, kwa mkopo kwa kipindi
chote cha msimu kilichosalia .
3. Spurs inafikiria kumsaini
kiungo mchezeshaji wa Borussia Monchengladbach na Ujerumani Florian Neuhaus,
23, kama mtu atakeyechukua nafasi yake.
4. Thomas Tuchel amedaiwa
kutopoteza muda katika mipango ya siku za usoni ya Chelsea kama mkufunzi wa
klabu hiyo. Raia huyo wa Ujerumani ambaye alichukua mahala pake Frank Lampard
katika uwanja wa Stamford Bridge siku ya Jumanne amesema beki wa klabu ya RB
Leipzig na Ufaransa Dayot Upamecano, 22, ni miongoni mwa wachezaji anaowalenga
sana.
5. Kufutwa kwa Lampard kumeiwacha klabu ya West Ham ikiwa na matumaini kwamba hamu ya Chelsea ya kumsajili mchezaji huyo wa England mwenye umri wa miaka 22 itakuwa imeisha.
EmoticonEmoticon