Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Alhamisi January 28

 

Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi January 28, 2021

1. Paris St-Germain 'imekosa heshima' katika kusaka saini ya kiungo mchezeshaji wa Argentina Lionel Messi, 33, kulingana na rais wa Barcelona Joan Laporta, ambaye ametishia kuiripoti klabu hiyo ya Ligue 1 kwa Fifa. 

2. Kiungo wa kati wa Ufaransa France Paul Pogba, 27, anasema kwamba atafanya mazungumzo na Man United mwisho wa msimu huu ili kutoa suluhu ya kudumu kuhusu hatma yake katika uwanja wa Old Trafford.

3. Kiungo wa kati wa Tottenham na England Dele Alli anafikiria kujiunga na Paris St-Germain, lakini mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy hataki mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kuondoka. 

4. Manchester City wamekubali kumuuza beki wa Uhispania Eric Garcia, 20,kwa Barcelona na mchezaji huyo atalazimika kucheza bila malipo kwa miezi sita ili kuweza kuhamia katika klabu hiyo anasema rais Victor Font. 

5. West Ham huenda ikasitisha hamu yao ya mshambuliaji mpya katika dirisha la uhamisho iwapo itafanikiwa kumsajilki kwa mkopo winga wa Man United na England Jesse Lingard, 28. 


EmoticonEmoticon