Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatano January 06

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano January 6, 2021

1. Kiungo wa kati wa Arsenal raia wa Ujerumani Mesut Ozil, 32, anafanya mazungumzo na DC United kuhusu kuhamia klabu hiyo ya Major League Marekani.

2. Mlinzi wa Uhispania Sergio Ramos, 34, amekataa ofa ya kuongezwa mkataba wa mwaka mmoja na Real Madrid, ambayo haitaki kwenda kinyume na sera yao ya kutoa makubaliano zaidi ya 30 ya muda huo kwa wachezaji wake.

3. Kocha wa Manchester City Pep Guardiola ana uhakika wa asilimia mia moja kuwa kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne atatia saini makubaliano mapya na klabu hiyo, licha ya taarifa kuwa mchezaji huyo, 29, amepanga kukataa ofa ya mkataba wao.

4. Tottenham Hotspur imesitisha mazungumzo na washambuliaji wa England Harry Kane, 27, na yule wa Korea Kusini Son Heung-min, 28, kutokana na janga la virusi vya corona.

5. Kocha wa Barcelona Ronald Koeman anasema ametengeneza orodha ya wachezaji "ambao itakuwa bora wakipatikana".


EmoticonEmoticon