Chelsea
imeamuajiri aliyekuwa mkufunzi wa Paris St-Germain Thomas Tuchel kuwa meneja
wake mpya kwa kandarasi ya miezi 18 kukiwa na fursa ya kuongeza kandarasi hiyo
itakapokamilika.
Alishinda mataji mawili ya ligi , kombe la Ufaransa na kombe
la ligi ya Ufaransa akiifunza PSG.
''Siwezi kusubiri kukutana na timu yangu mpya na kuanza ushindani
katika ligi yenye ushindani mkubwa katika soka. Nashukuru kuwa mmoja wa
wanafamilia wa Chelsea'', alisema Tuchel mwenye umri wa miaka 47.
Chelsea ilimfuta kazi meneja Lampard siku ya Jumatatu baada
ya kipindi cha miezi 18 , baada ya kuandikisha ushindi mmoja pekee katika mechi
tano za ligi ya Premia.
"Sote
tunaheshimu kazi ya Lampard na heshima aliyowacha katika klabu ya
Chelsea," aliongezea Tuchel.
Raia huyo wa Ujerumani sasa atakuwa mkufunzi 11 aliyeajiriwa
na mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich tangu bilionea huyo kununua klabu hiyo.
Mkurugenzi wa Chelsea Marina Granovskaia alimtaja Tuchel kama
mmoja wa makocha bora zaidi barani Ulaya , akiongezea kwamba bado kuna mengi ya
kuangazia katika msimu huu na siku za usoni.
Ataanza kusimamia klabu hiyo katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Wolves leo siku ya Jumatano.
EmoticonEmoticon