Idadi Ya Waliokufa Nchini Iraq Kwenye Shambulizi La Mabomu Yafikia 32

 

Idadi waliokufa kutokana na mashambulizi mawili ya kujitoa muhanga kwenye mji mkuu wa Iraq, Baghadad, imepanda na kufikia watu 32 huku wengine zaidi ya 110 wamejeruhiwa. 

Msemaji wa jeshi la nchi hiyo amearifu kuwa washambuliaji wawili waliovalia mikanda ya mabomu walijilipua mapema leo ndani ya soko lenye msongamano mkubwa katikati ya mtaa wenye shughuli nyingi mjini Baghdad. 

Shuhuda mmoja wa tukio hilo amesema mshambuliaji wa kwanza alijifanya mgonjwa huku akilia kwa sauti na alijilipua muda mfupi baada ya watu kumzingira kwa lengo la kumsaidia. 

Umoja wa Mataifa, Marekani, Uturuki, Jordan, Misri pamoja na kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis wamelaani shambulizi hilo la kikatili. Maafisa wa polisi na wahudumu wa hospitali wamesema idadi ya vifo inaweza kuongezeka kwa sababu wale waliojeruhiwa wamo kwenye hali mahututi.


EmoticonEmoticon