India Yaanza Kutoa Chanjo Ya Corona

 

India, taifa lenye idadi ya watu wapatao bilioni 1.3 leo imeanza mchakato wa kutoa chanjo dhidi ya virusi vya corona. 

Watu wapatao milioni 300 wanatarajiwa kupigwa sindano hiyo ya chanjo ifikapo mwezi Julai mwaka huu. 

Watakaopewa chanjo mwanzo ni wahudumu wa afya wapatao milioni 30, pamoja na wafanyakazi wengine wanaotoa huduma muhimu. 

Watakaofuatia ni wale waliopindukia miaka 50 na wenye matatizo ya kiafya ambao idadi yao inategemewa kuwa zaidi watu milioni 270. 

Utaratibu huo wa kwanza wa kutoa chanjo umeigharimu serikali ya India dola milioni 4.5. 

Chanjo hizo zinatengenezwa na kampuni mbili tofauti za madawa. AstraZeneca ambayo ni chanjo ya Chuo Kikuu cha Oxford inatengenezwa India na Tasisi ya Serum chini ya jina jipya la Covishield. 

Na ya pili iitwayo Covaxin inatengenezwa na kampuni ya madawa ya India ya Bharat Biotech Limited.


EmoticonEmoticon