Indonesia: Sehemu Za Miili Ya Watu Zapatikana Kwenye Pwani Baada Ya Ajali Ya Ndege

 

Nchini Indonesia, sehemu za miili ya watu waliohusika kwenye pwani ya ndege zimeopolewa katika kisiwa cha Jakarta Mahala ambapo ndege iliyokuwa imebeba abiria 62 ilianguka muda mfupi baada ya kuruka. 

Msemaji wa polisi Yusri Yunus amesema, leo Jumapili asubuhi, kuwa wamepokea mifuko miwili mmoja ukiwa na sehemu hizo za mwili na mwingine ukiwa na mali zinazoaminika kuwa ni za abiria.

Mamlaka nchini Indonesia imesema rada ya kufwatilia ndege inaonyesha kuwa ndege hiyo aina ya Boeing 737-500 ilianguka baharini takriban dakika nne baada ya kuondoka kutoka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Soekarno-Hatta mjini Jakarta. 

Ilikuwa inaelekea kwenye mji wa Pontianak ulio katika kisiwa cha Borneo. Safari ya ndege hiyo ilitegemewa kuchukua muda wa dakika 90 juu ya usawa wa bahari ya Java.

Waziri wa uchukuzi wa Indonesia Budi Karya Sumadi amewaambia waandishi wa habari kuwa ndani ya ndege hiyo walikuwemo watu hao 62 miongoni mwao wahudumu wa ndege pamoja na watoto 10. 

Waziri Sumadi amesema ndege hiyo ilichelewa kwa saa moja kabla ya kuruka na ilipoondoka mwendo wa saa nane na dakika 36, dakika nne baadaye, ikapotea kutoka kwenye Rada baada ya rubani kutoa mawasiliano kwa kitengo cha udhibiti wa safari za anga kuwa anaruka umbali wa futi 29,000 usawa wa bahari.


EmoticonEmoticon