lon
Musk amekuwa
tajiri wa kwanza duniani huku thamani yake ikipita dola bilioni 185 (Tsh
trilioni 428.83). Mfanyabiashara huyo ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Tesla na SpaceX amechukua
nafasi ya kwanza baada ya hisa zake za kampuni ya Tesla kuongezeka Alhamisi.
Amechukuwa
nafasi ya kwanza na kumpiku mwasisi wa kampuni ya Amazon Jeff Bezos ambaye
amekuwa akiorodheshwa wa kwanza kwa utajiri tangu mwaka 2017.
Thamani ya
Bwana Musk mmiliki wa kampuni ya magari yanayotumia umeme ya Tesla imeongezeka
mwaka huu na Jumatano ilifika dola bilioni 700 kwa mara ya kwanza.
Hatua hiyo
inafanya kampuni yake ya magari anayomiliki thamani yake kuwa ya juu hata
kushinda kampuni za Toyota, Volkswagen, Hyundai, GM na Ford kwa pamoja.
Musk
alisherehekea taarifa hizo kwa aina yake, akimjibu mtumiaji mmoja wa Twitter
aliyekuwa ameshirikisha wengine taarifa hizo kwa kuandika “inashangaza sana”.
Ujumbe wa awali uliokuwa juu ya ule wake uliangazia maoni juu ya utajiri wake.
“Karibu
nusu ya pesa zake zimepangiwa kutatua matatizo ya dunia, na nusu yake
zitasaidia kuwa na mji wenye kujitosheleza katika sayari ya mihiri yaani Mars,
kuhakikisha uendelezaji wa maisha kwa spishi zote pengine ikifika wakati dunia
idondokewe na kimondo kama vile dinosauri au kutokee Vita vya Tatu vya Dunia na
pengine tujimaliza,”
taarifa yake imesema.
Utajiri wa
Musk umeongezeka kwasababu ya siasa za Marekani ambapo Democrats itakuwa na
udhibiti wa bunge la Seneti katika kikao kijacho.
Daniel Ives,
mchambuzi wa kampuni ya soko la hisa la Wedbush aliandika: “Kikosi cha Seneti cha Democratic ni
imara na chenye uwezo wa kuleta mabadiliko kwa Tesla na sekta nzima ya magari
yanayotumia umeme kwa ujumla, kukiwa na uhakika wa kuangazia zaidi ajenda za
upunguzaji wa hatari ya mazingira katika kipindi cha miaka michahe ijayo.”
Utajiri wa Bezos pia
umekuwa ukiongezeka katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Janga la corona
limefaidi kampuni ya Amazon kwasababu ya kuongezeka kwa mahitaji ya manunuzi ya
mtandaoni na huduma za kukusanya na kutunza data.
Hata hivyo, alitoa asilimia 4 ya mapato ya biashara zake na kumpa aliyekuwa mke wake ambaye wametengana MacKenzie Scott hatua iliyomsaidia Musk kumpiku. Pia uwepo wa tishio la udhibti ni sawa na kusema kumechangia hisa za Amazon kutoongezeka sana kama ambavyo ingetarajiwa.
EmoticonEmoticon