Rais wa
Marekani Joe Biden ametengua marufuku ya ufadhili wa fedha ambazo zimekuwa
zikitumwa katika makundi ya kimataifa ya misaada ambayo husaidia katika suala
la kuavya mimba.
Amesema kwamba kukamilika kwa sera ya mji wa Mexico
kunatengua hatua ya rais Trump kuwanyima wanawake haki yao ya kiafya.
Barua hiyo inaagiza kubadilishwa kwa sera za enzi ya Trump
iliozuia ufadhili katika kliniki za Marekani ambazo hutoa rufaa ya uavyaji
mimba. Bwana Biden pia alisaini amri ya kupanua mpango wa bima ya afya ya
Obamacare.
"Sianzisha sheria mpya yoyote, ama jambo jipya la
sheria," alisema katika ofisi yake mnamo Alhamisi, akijibu kukosolewa
kwamba alikuwa akiongoza kwa kutoa amri badala ya kufuata sheria za bunge.
''Hakuna kitu kipya tunachofanya hapa mbali na kurudisha bima ya afya ya bei nafuu ...kama ilivyokuwa hapo awali kabla Trump kuwa rais'', aliongezea.
EmoticonEmoticon