Rais wa
Marekani Donald Trump amesaini amri ya rais ya kupiga marufuku kampuni nane za
China zenye program ya kutoa huduma ya ulipiaji wa bidhaa kwa njia ya mtandao.
Programu hizo ni pamoja na ile maarufu ya mtandao wa Alipay inayomilikuwa
na mfanyabiashara tajiri China Jack Ma, QQ Wallet na WeChat pay.
Amri hiyo
inaanza kutekelezwa ndani ya siku 45 baada yar ais kusema kuwa programu hizo
zinapigwa marufuku kwasababu ni tishio kwa usalama wa taifa la Marekani.
Inasemekana kuwa kuna uwezekano program hizo zinatumika
kufuatilia na kupata data za raia wa Marekani.
Programu zingine zilizopigwa marufuku ni pamoja na Tencent
QQ, CamScanner, SHAREit, VMate na WPS Office.
"Marekani lazima ichukue hatua madhubuti dhidi ya
waliotengeneza na kudhibiti programu za China kulinda usalama wa taifa
letu," Amri hiyo ya rais imesema.
Aidha, amri hiyo ya Rais Trump inasema "kwa kufikia bidhaa za elektroniki za simu aina ya smartphones, tablets, na kompyuta, programu za China zinaweza kufikia taarifa muhimu za watumiaji ikiwemo taarifa nyeti za utambulisho na taarifa za kibinafsi."
EmoticonEmoticon