Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amesema watu Milioni 2 wamefariki dunia
kutokana na ugonjwa wa virusi vya corona au COVID-19.
Kupitia
ujumbe wake aliotoa kwa njia ya video, Guterres amesema nyuma ya takwimu hizo
ni majina ya watu na nyuso zao.
“Tabasamu zao zimesalia historia, viti walivyokuwa wanaketi
wakati wa mlo wa usiku sasa ni vitupu, na vyumba sasa vimebakia na mwangwi wa
ukimya wa wapendwa wetu,” Gutteres
Katibu Mkuu
amesema cha kusikitisha zaidi, madhara ya janga la corona yamekuwa mabaya zaidi
kutokana na ukosefu wa juhudi za pamoja za kimataifa.
Ni kwa
mantiki hiyo amesema katika kukumbuka watu hao milioni 2 waliopoteza maisha
kutokana na corona, dunia inapaswa kuchukua hatua kubwa zaidi za pamoja na kwa
mshikamano.
“Lazima tuazimie kuhakikisha kuwa chanjo hizo zinaonekana kuwa jambo jema kwa umma wa kimataifa, chanjo za watu. Hii inahitajia ufadhili kamilifu wa kufanikisha mpango wa pamoja wa kuhamasisha na kusambaza chanjo dhidi ya Corona, au COVAX ambao umejipambanua kuhakikisha kuwa chanjo zinaweza kupatiwa kila mtu,” Guterres.
EmoticonEmoticon