Kenya imeagiza dozi milioni 24 za
chanjo ya COVID-19 ya kampuni ya AstraZeneca, Waziri wa Afya Kenya Mutahi Kagwe
amesema dozi hizo zinatarajiwa kuwasili Nchini humo wiki ya pili ya mwezi
Februari mwaka huu.
Taifa hilo lenye jumla ya Watu milioni 47, limerekodi jumla
ya maambukizi 97,398 na vifo 1,694 kutokana na virusi hivyo.
Uchumi wake pia umetikiswa kutokana na athari za janga la
COVID-19, Mutahi Kagwe amesema wahudumu wa afya ndio watapewa kipaumbele pamoja
na watoaji huduma nyingine za msingi mfano walimu.
Mutahi Kagwe amenukuliwa na gazeti la The Standard akisema
chanjo hiyo inatarajiwa mwezi ujao, Afisa mmoja katika Wizara ya Afya
amethibitisha kuwa taarifa hiyo ni kweli.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon